RUAHA CATHOLIC UNIVERSITY

Ruaha Catholic University Journal of Education and Development (RUCUJED)

RESEARCH ARTICLE
descriptionPDF
Urasimishaji wa Maneno ya Mkopo kutoka Kiswahili katikaLugha yaKimalila
Year 2021, Volume: 1, Issue: 1, 185-215, 2021-03-09
Azimio Sote
Ikisiri
Makala haya yamejikita katika kuchambua michakato inayotumika kurasimisha nomino za mkopo katika lugha ya Kimalila [M 24] zinazotoka katika lugha ya Kiswahili kwa kumakinika katika vipengele vya kifonolojia na kimofolojia. Data za utafiti huu zilikusanywa kwa njia ya hojaji na ushiriki, ambapo jumla ya maneno 312 yalichunguzwa. Makala yameonesha kwamba nomino zote zinazokopwa kutoka lugha ya Kiswahili kwenda lugha ya Kimalila ni lazima ziboreshwe walau kwa kuwekewa toni na kiambishi awali tanglizi. Mabadiliko mengine yaliyobainika ni ya udondoshaji na uchopekaji wa sauti pamoja na uambishaji wa maumbo ngeli mawili katika shina moja. Maboresho haya yanafanyika ili yaendane na fonolojia pamoja na mofolojia ya lugha ya Kimalila. Inaonesha kuwa hakuna neno la mkopo kutoka lugha ya Kiswahili linalorasimishwa bila kuboreshwa. Hata hivyo, kuwepo kwa maneno mengi ya Kiswahili katika lugha ya Kimalila kunaweza kuwa na athari katika uhai wa lugha Kimalila. Ipo haja ya tafiti zaidi kufanyika kuhusiana na athari za lugha ya Kiswahili au lugha nyingine katika lugha ya Kimalila.
Maneno Muhimu
Kiswahili, Kimalila, maneno ya mkopo, nomino, michakato ya urasimishaji
Details

Primary Language
Kiswahili

Subjects

Journal Section
Research Article

Authors
Azimio Sote

Publication Date
2021-03-09

Submission Date
0000-00-00

Acceptance Date
0000-00-00

Cite

APA
Azimio Sote. (2021). Urasimishaji wa Maneno ya Mkopo kutoka Kiswahili katikaLugha yaKimalila. Ruaha Catholic University Journal of Education and Development, 1(1), 185-215.content_copy

Copyright © 2025 RUCU, All Rights Reserved.