RESEARCH ARTICLE
descriptionPDFTathmini Kuhusu Sera na Dhamira ya
Ujamaa Nchini Tanzania
Year 2021, Volume: 7, Issue: 2, 74-79, 2016-12-02
Abel Nyamahanga
Ikisiri
Makala hii imechunguza sera na dhamira ya
ujamaa nchini Tanzania. Data za msingi
zilizotumika katika makala haya zilipatikana
maktabani kwa mbinu ya usomaji makini.
Matini mbalimbali zilichunguzwa ili kupata
data za msingi. Uchambuzi na mjadala wa
data zilizowasilishwa katika makala hii
umeongozwa na nadharia ya Uhalisia.
Matokeo katika makala hii yanaonesha kuwa
misingi ya sera za Azimio la Arusha na ujenzi
wa Ujamaa wa Tanzania ulikabiliwa na
masuala mbalimbali yaliyoaathiri utekelezaji
wake. Mkakati wa kuwahamisha wananchi
kwa nguvu katika vijiji vya maendeleo
ulipingana na haki za binadamu kwa kuwa
baadhi ya viongozi walitumia nguvu kupita
kiasi. Pia, uliathiri kilimo cha mazao ya
kudumu ya biashara katika baadhi ya mikoa.
Azimio la Arusha lilionekana kuwa ni sera
iliyoshindwa kufanya kazi na kuleta
maendeleo. Makala hii inahitimisha kuwa
Azimio la Arusha lilifumbata itikadi, dira na
mwongozo wa taifa. Azimio la Arusha
lilihitaji kufanyiwa marekebisho ili liendane
na mazingira ya sasa ya ulimwengu badala ya
kulitupa kabisa. Tatizo kubwa lililopo sasa ni
kwamba kila awamu ya uongozi unakuwa na mtazamo na mwelekeo binafsi wa
kuendesha nchi.
Maneno Muhimu
Azimio la Arusha, Sera za Azimio la Arusha, Dhamira za Azimio
la Arusha na Ujamaa wa Tanzania.
Details
Primary Language
Kiswahili
Journal Section
Research Article
Publication Date
2016-12-02
Submission Date
0000-00-00
Acceptance Date
0000-00-00
Cite