RESEARCH ARTICLE
descriptionPDFMchango wa Lugha Asili za Wabantu katika Kuendeleza
Historia ya Lugha ya Kiswahili
Year 2021, Volume: 1, Issue: 2, 217-228, 2021-09-08
Abel Nyamahanga
Ikisiri
Makala haya yamechunguza mchango wa lugha asili za
Kibantu katika kuendeleza historia ya lugha ya Kiswahili.
Makala haya ni matokeo ya kuwepo kwa hoja za wataalamu
mbalimbali zinazosigana kuhusu Ubantu wa lugha ya
Kiswahili. Uchunguzi, katika makala haya, umefanywa kwa
kujikita katika misingi ya ushahidi wa kiisimu. Ushahidi wa
kiisimu umefanyika kwa kuzingatia uchunguzi wa lugha ya
Kiswahili katika mfumo mzima wa historia ya mgawanyiko wa
kusambaa kwa lugha za Kibantu. Ushahidi wa data za kiisimu
umerejelewa kwa kuzingatia mwachano na umbali wa
kijiografia baina ya jamiilugha moja na nyingine kutoka katika
baadhi ya lugha za Kibantu kutoka nchini Tanzania, Zambia na
Burundi ili kuthibitisha Ubantu wa lugha ya Kiswahili. Data za
msingi za makala zilikusanywa kwa mbinu za uwandani na
maktabani. Mbinu ya mahojiano ilitumika kupata data za
msingi. Mapitio ya nyaraka zilizotumika kufafanua na
kuthibitisha data za msingi yalipatikana kwa mbinu za usomaji
wa nyaraka zilizopo maktabani na mtandaoni. Makala haya
yanahitimisha kuwa Kiswahili ni mojawapo ya lugha katika
jamii kubwa ya lugha za Kibantu.
Maneno Muhimu
Kiswahili, Lugha za Kibantu, IsimuLinganishi, Isimu-Historia na Ushahidi wa Kiisimu
Details
Primary Language
Kiswahili
Journal Section
Research Article
Publication Date
2021-09-08
Submission Date
0000-00-00
Acceptance Date
0000-00-00
Cite