RESEARCH ARTICLE
descriptionPDFMdhihiriko wa Vionjo vya Fasihi ya Kisasa
katika Nyimbo za Taarabu
Year 2021, Volume: 7, Issue: 2, 1-10, 2016-12-02
Hassan, R. Hassan
Abstract
Makala hii inahusu mdhihiriko wa vionjo vya
fasihi ya kisasa katika nyimbo teule za
Taarabu. Data za msingi zilizofafanuliwa
katika makala hii zimepatikana maktabani
kwa kutumia njia ya uchanganuzi wa matini.
Nadharia ya Usasa imetumika kama kiunzi
muhimu katika ukusanyaji, uchambuzi na
mjadala wa data zilizowasilishwa katika
makala hii. Makala imebaini kuwa nyimbo za
Kiswahili za Taarabu zina ukwasi wa vionjo
ambavyo vinaziweka katika kapu la fasihi ya
kisasa. Vionjo hivyo ni pamoja na mwanzo
wenye kiitikio chenyesauti kali na zenye
vishindo, matumizi ya mbinu ya cheba,
matumizi ya maneno ya mtaani na matumizi
ya nyenzo za kisayansi na kiteknolojia.
Nyimbo hizi zimekuwa zikitumia mashairi ya
mipasho, mwingiliano wa wimbo ndani ya
wimbo, kuchanganya ndimi na kuhitimishwa
na sehemu ya ngoma chini. Makala hii
inahitimisha kwamba nyimbo za Kiswahili za
Taarabu zimefumbata vionjo vya kisasa
ambavyo vinazifanya kuwa na mabadiliko
makubwa na kuzidi kujiimarisha kwa hadhira
ya sasa.
Keywords
Vionjo, Nyimbo, Fasihi ya Kisasa na Nyimbo za Taarabu.
Details
Journal Section
Research Article
Publication Date
2016-12-02
Submission Date
0000-00-00
Acceptance Date
0000-00-00
Cite