RESEARCH ARTICLE
descriptionPDFUsawiri wa Lugha ya Ishara Iliyotafsiriwa katika
Shetani Msalabani
Year 2022, Volume: 1, Issue: 1, 66-76, 2022-02-10
Birigitha Ngwano John
Ikisiri
Makala hii inasawiri lugha ya ishara iliyotafsiriwa
katika riwaya ya Shetani Msalabani. Mbinu ya
usaili na usomaji matini zilitumika kupata data za
msingi zilizotumika katika makala hii. Data za
msingi zilipatikana kwa kurejelea riwaya ya Shetani
Msalabani na matini chanzi yake ambayo ni Devil
on the Cross. Nadharia ya Ulinganifu wa
Kimawasiliano imetumika kama kiunzi cha
uchambuzi wa data zilizowasilishwa katika makala
hii. Makala hii imebaini kuwa lugha ya ishara
iliyotafsiriwa katika Shetani Msalabani
imejibainisha kupitia vipengele vya wahusika wa
kiishara, matukio ya kiishara na katika kichwa cha
riwaya. Makala hii inapendekeza kuwa wafasiri wa
kazi za kifasihi wanapaswa kuzingatia misingi ya
kiulinganifu katika kutafsiri lugha ya ishara ambayo
ni kipengele muhimu cha matumizi ya lugha.
Maneno Muhimu
Tafsiri, ishara, lugha ya ishara,
usawiri wa lugha na ulinganifu wa kimawasiliano
Details
Primary Language
Kiswahili
Journal Section
Research Article
Authors
Birigitha Ngwano John
Publication Date
2022-02-10
Submission Date
0000-00-00
Acceptance Date
0000-00-00
Cite