RESEARCH ARTICLE
descriptionPDFFaida za Utumizi wa Ramani ya Dhana
katika Kufundishia Msamiati wa Kiswahili
Shule za Msingi
Year 2021, Volume: 7, Issue: 2, 29-42, 2016-12-02
Tumaini Samweli Mugaya
Ikisiri
Makala hii imechunguza kuhusu faida za
utumizi wa ramani ya dhana katika
kufundishia kiswahili shule za msingi mkoani
Dodoma. Mbinu za usaili na ushuhudiaji
zimetumika kupata data za msingi. Data za
msingi zilichambuliwa kwa kutumia mkabala
wa Kitaamuli. Nadharia ya Ujenzi wa Maana
ya Vygotsky imetumika katika kujadili
masuala mbalimbali na kutoa picha halisi ya
faida za utumiaji wa ramani ya dhana katika
ufundishaji wa msamiati. Matokeo ya makala
hii yameonesha kuwa kuna uhusiano mkubwa
kati ya matumizi ya ramani ya dhana na
ufundishaji wa misamiati ya lugha. Baadhi ya
faida za kutumia ramani ya dhana kutafuatia
maarifa ya awali ya mwanafunzi ni kupata
maarifa ya maana elekezi, kutathmini
kiwango cha uelewa wa mwanafunzi,
kuwezesha utungaji wa msamiati, kujenga
tajiriba ya kujieleza wakati wa ufundishaji na
ujifunzaji wa msamiati na kutumika kama
zana ya kufundishia na kujifunzia. Makala hii
inapendekeza kuwa ramani ya dhana ni
mbinu bora si tu inajenga uwezo mkubwa
kwa wanafunzi katika kujifunza msamiati wa
Kiswahili, bali ni mbinu yenye ufanisi
mkubwa wa kutolea maarifa katika ufundishaji wowote.
Maneno Muhimu
Lugha, Msamiati, Ramani ya Dhana na Kiswahili.
Details
Primary Language
Kiswahili
Journal Section
Research Article
Authors
Tumaini Samweli Mugaya
Publication Date
2016-12-02
Submission Date
0000-00-00
Acceptance Date
0000-00-00
Cite