RESEARCH ARTICLE
descriptionPDFHali na Hadhi ya Mwanamke katika
Fasihi ya Kiswahili
Year 2021, Volume: 7, Issue: 2, 11-19, 2016-12-02
Willy Migodela & Abel Nyamahanga
Ikisiri
Makala hii imechunguza hali na hadhi ya
mwanamke kwa kurejelea riwaya ya Dunia
Uwanja wa Fujo. Data za msingi
zilizotumika katika makala zilipatikana kwa
mbinu ya usomaji makini. Mbinu ya uteuzi
lengwa ilitumika kupata data za msingi
kutoka katika riwaya teule. Uchambuzi na
mjadala wa data zilizowasilishwa katika
makala hii umeongozwa na nadharia ya
Ufeministi. Matokeo katika makala hii
yanaonesha kuwa mwanamke amebainishwa
katika nafasi mbalimbali zinazohusu malezi,
utoaji wa maamuzi, ulaghai na usaliti katika
mapenzi na ndoa. Mtazamo hasi
unaodokezwa kuhusu mwanamke
unasababishwa na harakati za mwanaume
zinazowabana na kuwatumbukiza wanawake
kufikia hapo walipo. Makala hii
inahitimisha kuwa jamii inatakiwa kuchukua
hatua za msingi za kuondokana na jambo
linalowadhalilisha na kuwafanya wanawake
wapuuzwe na kutazamwa katika udhaifu.
Mwanamke hana budi kujijengea misingi
imara ya kujitegemeana kufanya shughuli
halali zenye tija ili kuiendeleza na
kuidumisha heshima anayostahili katika
jamii na taifa lake.
Maneno Muhimu
Hali, Hadhi, Mwanamke, Ufeministi na Fasihi ya Kiswahili
Details
Primary Language
Kiswahili
Journal Section
Research Article
Authors
Willy Migodela & Abel Nyamahanga
Publication Date
2016-12-02
Submission Date
0000-00-00
Acceptance Date
0000-00-00
Cite