RESEARCH ARTICLE
descriptionPDFNafasi ya Misemo katika Jamii ya Wairaqw nchini
Tanzania
Year 2021, Volume: 1, Issue: 2, 180-196, 2021-09-08
Asha Shaaban
Ikisiri
Makala haya yamechunguza dhamira za misemo katika jamii
ya Wairaqw nchini Tanzania kwa kudokeza namna mifumo ya
maisha ya jamii inavyoakisiwa katika kazi za kifasihi kwa
kurejelea utanzu teule wa misemo ya jamii ya Wairaqw hapa
nchini. Data za msingi zilikusanywa katika misemo ya jamii ya
Wairaqw kwa mbinu za mahojiano na majadiliano. Lugha za
Kiswahili na Kiiraqw zilitumika katika mahojiano,
majadiliano na unukuzi wa data. Mbinu ya uteuzi lengwa
ilitumika kupata watafitiwa waliosaidia kupata na kutafsiri
data zilizokusanywa. Uchambuzi na mjadala wa data
zilizowasilishwa umeongozwa na nadharia ya Usosholojia.
Dhamira zilizochunguzwa hutumika kama maktaba mahsusi
ya urejelezi wa masuala ya kijamii na kiungo thabiti cha
kiasili kinachojenga mfumo wa kuifunza, kuiimarisha na
kuiweka jamii pamoja katika misingi ya utamaduni na falsafa
nzima ya maisha tangu kale mpaka sasa. Mwisho, misemo ni
matendo ya msingi ya binadamu; na ni mojawapo ya vyombo
thabiti vya kijadi vinavyopewa uwanja mpana katika
kutekeleza, kuongoza na kutoa elimu kuhusu tabia na
mienendo inayohitajika katika jamii.
Maneno Muhimu
Jamii ya Wairaqw, misemo, Tanzania
Details
Primary Language
Kiswahili
Journal Section
Research Article
Publication Date
2021-09-08
Submission Date
0000-00-00
Acceptance Date
0000-00-00
Cite