RESEARCH ARTICLE
descriptionPDFUsawiri wa Nafasi ya Mwanamke Katika Malezi: Mifano Kutoka Katika Nyimbo Teule za
Bongo Fleva
Year 2024, Volume: 3, Issue: 1, 64-86, 2024-10-02
Venance Gilbert Mpate
Ikisiri
Malezi ni jambo la muhimu sana katika jamii yoyote. Ni mchakato wa muda mrefu ambao
huhusisha mzazi ama mlezi na mtoto katika makuzi yake. Katika jamii za Kiafrika suala la
malezi hufanywa kwa kiasi kikubwa na wanawake. Makala haya yanakusudia kuchunguza
usawiri wa nafasi ya wanawake katika malezi katika jamii. Makala yameongozwa na Nadharia
za Ufeministi wa Kiafrika na Mwingilianomatini. Data zimepatikana kwa njia ya udurusu matini
kwa kusikiliza mashairi ya nyimbo za Bongo fleva katika mtandao wa YouTube. Mbinu
iliyotumika kupata nyimbo zilizotafitiwa ni usampulishaji lengwa ambapo mtafiti alisikiliza
nyimbo nyingi na kupata jumla ya nyimbo kumi na saba za Bongo fleva zinazozungumzia nafasi
ya mwanamke katika malezi ya watoto. Data katika makala haya zimefafanuliwa kwa njia ya
maelezo. Utafiti ulibaini kuwepo mchango mkubwa unaofanywa na wanawake katika malezi
kwenye jamii kama ulivyosawiriwa katika nyimbo teule za Bongo fleva. Pia utafiti ulijielekeza
katika kuangalia athari hasi za kukosekana kwa nafasi ya mama2
katika malezi na makuzi ya
mtoto.
Maneno Muhimu
Bongo fleva, malezi, usawiri.
Details
Primary Language
Kiswahili
Journal Section
Research Article
Authors
Venance Gilbert Mpate
Publication Date
2024-10-02
Submission Date
0000-00-00
Acceptance Date
0000-00-00
Cite