RESEARCH ARTICLE
descriptionPDFUfungwa wa Kisaikolojia katika Riwaya ya Takadini
Year 2021, Volume: 1, Issue: 2, 197-216, 2021-09-08
Zuhura Said
Ikisiri
Makala haya yamechunguza suala la ufungwa wa kisaikolojia
katika riwaya ya Takadini. Tatizo hasa ni kwamba dhana ya
ufungwa ilichunguzwa zaidi na wataalamu waaliotangulia
katika mwegamo wa jela. Suala la ufungwa wa kisaikolojia
halikushughulikiwa kwa mapana yake. Hata hivyo, makala
yamejiegemeza katika mkabala wa kitaamuli. Data
zimepatikana kwa njia ya uchambuzi wa matini. Nadharia ya
Saikolojia Changanuzi imetumika katika uchambuzi wa data
zilizowasilishwa. Matokeo ya uchunguzi huu yameonesha kuwa
ufungwa wa kisaikolojia umegawanyika katika makundi makuu
mawili. Makundi hayo ni ufungwa wa kisaikolojia wa kijaala
na ufungwa wa kisaikolojia usio wa kijaala. Ufungwa wa
kisaikolojia wa kijaala ndio ambao umemakinikiwa zaidi
katika makala haya. Aina ya pili imedokezwa tu ili kujenga
msingi wa hoja. Aidha, matokeo ya uchunguzi yanadhihirisha
kuwa kila mwanadamu ni mfungwa kwa kuwa hakuna mwenye
uhuru uliokamilika. Hali hii inatokana na kukabiliwa na
mamlaka, kanuni, sheria au taratibu zinazompangia
mwanadamu asifanye baadhi ya mambo, ambayo anahisi
anawiwa kuyafanya. Makala yanahitimisha kuwa kila mtu
huangukia katika ufungwa wa aina mbalimbali kwa sababu ya
kushindwa kutimiza matamanio ya nafsi yake kwa namna
aitakayo. Matokeo yake hujikuta akiangukia katika
manungāuniko, mafumbo na kusema bila kuzingatia taratibu,
utamaduni na staha za jamii inayohusika.
Maneno Muhimu
Ufungwa wa kisaikolojia, nadharia ya
ufungwa, mkondo wa ufungwa na riwaya ya ufungwa
Details
Primary Language
Kiswahili
Journal Section
Research Article
Publication Date
2021-09-08
Submission Date
0000-00-00
Acceptance Date
0000-00-00
Cite