RESEARCH ARTICLE
descriptionPDFBibliakama Mgodi wa Fasihi ya Kiswahili: Mifano kutoka Tamthiliya Teule
za Emmanuel Mbogo
Year 2023, Volume: 8, Issue: 2, 35-50, 2023-02-02
Emmanuel Oscar Msangi
Ikisiri
Makala haya yanachunguza suala la Ubiblia katika tamthiliya teule za Emmanuel Mbogo. Data
za msingi za makala haya zimepatikana katika tamthiliya za Nyerere na Safari ya Kanaani
(2015) na Sadaka ya John Okello (2015). Ubiblia umeonyeshwa kwenye tamthiliya hizo kupitia
vipengele vyake vya kifani vinavyojitokeza katika kazi teule. Katika makala haya tumetumia
mbinu ya usomaji makini kwa kusoma na kuchunguza tamthiliya teule. Uchambuzi wa data
katika utafiti huu umefanywa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo. Nadharia ya
Mwingilianomatini ndiyo iliyotumika katika ukusanyaji, uchambuzi na mjadala wa data za
utafiti. Makala haya yamebaini kwamba kuna Ubiblia mwingi katika tamthiliya tafitiwa
alizoandika Emmanuel Mbogo.Ubiblia huo unajitokeza kupitia vipengele vya majina ya
tamthiliya, masimulizi ya Biblia, wahusika wa Biblia, nukuu za Biblia na mitindo ya Biblia.
Wasomaji wa kazi hizi waliopata kukutana na Biblia kabla, wakikutana na kazi hizo za kifasihi
wanabaini taswira za Biblia bila kiza chochote. Msomaji wa kazi hizi za fasihi atabaini kwamba
vipengele vya Biblia vilivyotumika katika tamthiliya teule vinaendana sawasawa na yale
yaliyojiri kwenye Biblia. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuna uhusiano kati ya kazi za fasihi za
Emmanuel Mbogo na yale yaliyoko katika Biblia.Makala haya yanahitimisha kuwa Ubiblia
unaojithihirisha katika Nyerere na Safari ya Kanaani na Sadaka ya John Okelloumehusisha
matukio halisi na matukio ya kazi nyingine za Kibiblia
Maneno Muhimu
Ubiblia, Fasihi ya Kiswahili, Nadharia ya Mwingilianomatini
Details
Primary Language
Kiswahili
Journal Section
Research Article
Authors
Emmanuel Oscar Msangi
Publication Date
2023-02-02
Submission Date
0000-00-00
Acceptance Date
0000-00-00
Cite