RESEARCH ARTICLE
descriptionPDFNafasi ya Fasihi - Mazingira Kuelekea Uchumi wa Viwanda Nchini Tanzania:
Mifano Kutoka Katika Nyimbo za Mrisho Mpoto na Beka Flavour
Year 2023, Volume: 8, Issue: 2, 51-59, 2023-02-02
Rose Sekile
Ikisiri
Makala haya yamechunguza nafasi ya fasihi mazingira katika kuelekea uchumi wa viwanda
nchini Tanzania. Data za msingi zilipatikana katika jamii kwa kuchunguza nyimbo zinazohusu
mazingira. Mbinu ya usomaji makini na upembuzi yakinifu zilitumika kupata data za msingi.
Mihimili ya nadharia ya Uhalisia na nadharia ya Ekolojia ndiyo iliyoongoza katika mjadala wa
uchanganuzi wa data zilizowasilishwa. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa kuna uhusiano
mkubwa kati ya mazingira na uendelezaji wa viwanda. Aidha, nyimbo ni nyenzo muafaka ya
kuelimisha jamii kuhusu utunzaji wa mazingira na kudhibiti mienendo na tabia isiyofaa katika
jamii. Utunzaji wa mazingira nchini Tanzania inaonekana ni jukumu la asasi zilizopewa
dhamana kuhusu mazingira na si jukumu la kila mmoja wetu. Makala haya yanapendekeza kuwa
ni vyema uelimishaji wa elimu mazingira ufanyike katika ngazi mbalimbali kuanzia ngazi ya
kaya hadi kitaifa ili kumfanya kila mmoja wetu awe sehemu ya utunzaji wa mazingira.
Uanzishwaji wa viwanda na ukuaji wa uchumi unatakiwa uende sanjari na uhaishaji wa
mazingira.
Maneno Muhimu
Mazingira, Fasihi - mazingira, ekolojia, uchumi na uchumi wa viwanda
Details
Primary Language
Kiswahili
Journal Section
Research Article
Publication Date
2023-02-02
Submission Date
0000-00-00
Acceptance Date
0000-00-00
Cite