RESEARCH ARTICLE
descriptionPDFUzingativu wa Utamaduni katika
Utayarishaji wa Matini Halisi za
Kujifunzia Lugha ya Pili
Year 2021, Volume: 7, Issue: 2, 53-61, 2016-12-02
Asia Mashaka Akaro
Ikisiri
Utafiti huu unachunguza umuhimu wa
Matini Halisi zinazoakisi utamaduni wa
lugha husika katika kujifunza Lg2. Utafiti
huu ni wa kimaktaba. Mbinu ya ukusanyaji
wa data iliyotumika ni uchanganuzi wa
nyaraka. Data za msingi zilikusanywa katika
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Utafiti huu
umebaini kuwa Matini Halisi za kufundishia
Lg2 lazima ziwe zimezingatia mazingira
yanayohusika ambamo zitatumika na
zichochee maingiliano na uzalifu. Pia,
zizingatie maumbo na dhima ya Lg2 na
shurti zifungamanishe stadi zote za lugha za
kusikiliza, kuzungumza, kusoma, kuandika
na utamaduni. Kwa upande wa mchango wa
Matini Halisi zilizozingatia utamaduni wa
lugha lengwa, mjifunzaji Lg2 anahusisha
moja kwa moja matini anayoitumia na kitu
anachojifunza. Mjifunzaji anapata uelewa
wa kujieleza kwa urahisi na anajifunza kwa
urahisi misamiati mipya kupitia maelezo au
ufafanuzi uliomo katika matini hizo.
Mjifunzaji wa Lg2 anapata motisha ya
kujifunza kupitia mtini hizo. Mjifunzaji wa
Lg2 hukuza stadi za lugha katika hali ya
ung‟amuzitambuzi. Makala yamehitimisha kwamba ili matini halisi ziwe na tija kwa
wajifunzaji shurti ziwe nyumbufu na kwenda na wakati.
Maneno Muhimu
Matini Halisi, Uhalisi wa Matini, Uhalisi wa Matini Kiuendelevu
na Uhalisi wa Matini Kimatumizi.
Details
Primary Language
Kiswahili
Journal Section
Research Article
Authors
Asia Mashaka Akaro
Publication Date
2016-12-02
Submission Date
0000-00-00
Acceptance Date
0000-00-00
Cite