RESEARCH ARTICLE
descriptionPDFDhima ya Usasanyuzi Dosari katika Ufundishaji na Ujifunzaji wa
Lugha ya Pili: Mifano ya Wajifunzaji wa Kiswahili katika Jamii ya
Wakinga Nchini Tanzania
Year 2023, Volume: 2, Issue: 1, 147-169, 2023-03-01
Arnold B. G. Msigwa
Ikisiri
Usasanyuzi dosari ni eneo muhimu katika taaluma ya isimu tumizi.
Vilevile, ni mbinu pangilifu ya kuchanganua dosari za mjifunzaji lugha.
Kitaaluma dosari si kitu kibaya bali ni kipengele muhimu sana katika
mchakato wa ujifunzaji lugha. Dosari husaidia kutambua mchakato
changamani wa maendeleo ya lugha na namna pangilifu ya kubaini,
kueleza na kufafanua dosari za mjifunzaji lugha. Pia, dosari zinaweza
kusaidia kutoa welewa wa mchakato wa kuamili Lugha ya pili. Makala
haya, kwa hiyo, yanalenga: kubainisha dosari zinazojitokeza kwa
wajifunzaji wa Kiswahili katika jamii ya Wakinga, sababu za wajifunzaji
wa lugha ya pili katika jamii ya Wakinga na kupendekeza mikakati ya
kupunguza hizo dosari. Baadhi ya dosari zilizobainika ni dosari za
undoshaji wa fonimu /h/, uchopekaji wa fonimu /u/ na dosari za
kimuundo; yaani ukosefu wa upatanisho wa kisarufi. Dosari hizi za
uchopekaji zimesababishwa na uhawilishaji wa kanuni za lugha ya
kwanza katika lugha ya Kiswahili; ambapo mjifunzaji wa lugha ya pili
amehamisha utaratibu wa lugha yake ya kwanza na kuutumia kwenye
lugha ya pili anayojifunza na kusababisha dosari. Aina hii ya uhawilishaji
ni uhawilishaji hasi. Makala yanahitimisha kwamba dosari hizi
zinachangiwa kwa kiasi kikubwa na lugha yao ya kwanza.
Maneno Muhimu
dosari, usasanyizi dosari na uhawilishaji
Details
Primary Language
Kiswahili
Journal Section
Research Article
Authors
Arnold B. G. Msigwa
Publication Date
2023-03-01
Submission Date
0000-00-00
Acceptance Date
0000-00-00
Cite