RESEARCH ARTICLE
descriptionPDFKutathmini athari za kimatamshi za kihaya kama lugha ya kwanza kwa wanaojifunza
kiswahili sanifu kama lugha ya pili
Year 2024, Volume: 9, Issue: 2, 53-71, 2024-12-29
Godfrey Ndaluhela
Ikisiri
Utafiti huu ulitathmini athari za matamshi za Kihaya kama lugha ya kwaza kwa wanaojifunza
Kiswahili sanifu kama lugha ya pili. Wataalamu wengi wanakubaliana kuwa lugha zinapokutana
huwa zinaathiriana. Utafiti ulifanyika katika mkoa wa Kagera katika wilaya ya Missenyi,
Tanzania. Mbinu zilizotumika kukusanya data ni hojaji na ushuhudiaji. Data za utafiti huu
zimechanganuliwa kwa mkabala wa kimaelezo na kuongozwa na Nadharia ya Lugha Kadirifu.
Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa, kuna athari za uchopekaji wa fonimu, udondoshaji wa
fonimu na kubadilisha fonimu. Aidha, Makala hii imeweka bayana mbinu zinazotumiwa na
walimu kuwasaidia wazungumzaji wa Kihaya kujifunza Kiswahili sanifu ambazo ni kusoma kwa
sauti, masahihisho kwa fonimu, nyimbo, kurudia rudia kutamka maneno, kutumia vielelezo na
michoro na kuwapatia wanafunzi kazi za kutafuta maneno yenye silabi husika.
Maneno Muhimu
Athari za matamshi, lugha ya Kihaya, lugha ya Kiswahili, sanifu
Details
Primary Language
Kiswahili
Journal Section
Research Article
Publication Date
2024-12-29
Submission Date
2024-10-15
Acceptance Date
2024-02-02
Cite