RUAHA CATHOLIC UNIVERSITY

Ruaha Catholic University Journal of Education and Development (RUCUJED)

RESEARCH ARTICLE
descriptionPDF
Ubunga Unavyoakisiwa katika Fasihi ya Kiswahili
Year 2021, Volume: 1, Issue: 1, 238-253, 2021-03-09
Gerephace Mwangosi
Ikisiri
Tamthiliya katika jamii na mazingira ya Afrika Mashariki inatumika kama chombo kinachomudu harakati mbalimbali za kijamii. Baadhi ya masuala yanayoelezwa ni mwingiliano na uhusiano wa kisanaa, kimaudhui na kiutamaduni unaoweza kuthibitishwa kupitia kazi za fasihi ya Kiswahili.Makala haya yamechunguza nafasi na usawiri wa Ubunga katika fasihi ya Kiswahili kwa kurejelea tamthiliya teule za Mfalme Juha na Amezidi. Ubunga katika sanaa unalenga kujenga misingi ya kuifunza na kuifikirisha jamii kwa kutumia mbinu ya ucheshi na kusisitiza uwazi kulingana na hali halisi ya uzoefu wa maisha ya binadamu na mazingira yake.Data za msingi za makala haya zimepatikana maktabani kwa kudurusu vitabu teule vilivyobainishwa. Mapitio ya nyaraka zilizotumika kuthibitisha data za msingi pia zimepatikana kwa mbinu za usomaji wa nyaraka. Nadharia ya Unafsia imetumika katika uchambuzi na mjadala wa data zilizowasilishwa.Makala yanahitimisha kuwa ubunga katika fasihi ni mojawapo ya vyombo muhimu vya kiharakati vinavyomudu mahitaji ya jamii kwa kuzingatia hali halisi ya mifumo na mitindo ya maisha ya binadamu.
Maneno Muhimu
Kaida, Ubunga, Muakiso, Unafsia
Details

Primary Language
Kiswahili

Subjects

Journal Section
Research Article

Authors
Gerephace Mwangosi

Publication Date
2021-03-09

Submission Date
0000-00-00

Acceptance Date
0000-00-00

Cite

APA
Gerephace Mwangosi. (2021). Ubunga Unavyoakisiwa katika Fasihi ya Kiswahili. Ruaha Catholic University Journal of Education and Development, 1(1), 238-253.content_copy

Copyright © 2025 RUCU, All Rights Reserved.