RESEARCH ARTICLE
descriptionPDFMchango wa Matumizi ya TEHAMA katika Ufundishaji wa Stadi ya Kusoma kwa
Wasambaa Wanaojifunza Kiswahili kama Lugha ya Pili
Year 2024, Volume: 3, Issue: 1, 15-26, 2024-10-02
Davian Buguna
Ikisiri
Matumizi ya TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji wa lugha yanaendelea kushamiri kote
duniani. Ukuaji wa teknolojia unasaidia kurahisisha na kuchagiza uelewa wa wajifunzaji katika
stadi mbalimbali za lugha. Makala haya yalilenga kudodosa maoni ya walimu wa Kiswahili
kama lugha ya pili wilayani Lushoto, kuhusu mchango wa TEHAMA katika ufundishaji wa stadi
ya kusoma kwa Wasambaa wanaojifunza Kiswahili kama lugha ya pili. Data za makala haya
zimekusanywa kwa njia ya usahili. Nadharia iliyotumika kuongoza utafiti huu ni modeli ya
Ukubalifu wa Teknolojia ya Devis (1989). Watoataarifa waliotumika ni walimu kumi (10) kutoka
katika shule tano (5) za msingi wilayani Lushoto mkoani wa Tanga. Mkabala wa kitaamuli
umetumika katika uchanganuzi wa data. Matokeo yanaonesha kuwa matumizi ya TEHAMA
yamekuwa na mchango mkubwa katika kurahisisha na kuboresha mbinu za kitamaduni za
ufundishaji wa stadi ya kusoma na wale wasiotumia TEHAMA wanaona kuwa matumizi ya
TEHAMA katika mazingira ya vijijini yana changamoto nyingi za kimazingira, kiujuzi na
kiuchumi ambazo hukwamisha mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji wa stadi ya kusoma.
Maneno Muhimu
Matumizi ya TEHAMA, ufundishaji, stadi ya kusoma
Details
Primary Language
Kiswahili
Journal Section
Research Article
Publication Date
2024-10-02
Submission Date
0000-00-00
Acceptance Date
0000-00-00
Cite