RUAHA CATHOLIC UNIVERSITY

Ruaha Catholic University Journal of Education and Development (RUCUJED)

RESEARCH ARTICLE
descriptionPDF
Kategoria ya Vimahali katika Lugha ya Kiswahili
Year 2021, Volume: 1, Issue: 1, 254-278, 2021-03-09
Fabiola Hassan
Ikisiri
Wanaisimu wa lugha ya Kiswahili wameainisha vimahali katika kategoria ya vielezi. Vimahali vinarejelea mahali tendo lilipotendeka, linapotendeka au litakapotendeka. Vilevile, ni vielezi kwa sababu vimeambikwa kiambishi tamati cha mahali –ni. Hata hivyo, matumizi ya vimahali katika tungo yanadhihirisha kuwa vina tabia za nomino. Makala haya yanabainisha kategoria ya vimahali katika Kiswahili kwa kuzingatia tabia zake za kisemantiki, kimofolojia na sintaksia kwa kuwa makala haya yanahusisha mofolojia, sintaksia na semantiki. Data za makala haya zimepatikana kwa mbinu ya uchambuzi wa matini mbalimbali za Kiswahili pamoja na upimaji wa usahihi wa kisarufi. Ufafanuzi wa data hizo umetumia nadharia ya Sampuli Kifani, ambayo inatoa fursa ya kuzichambua data zinazoonesha mwingiliano wa kikategoria pamoja na udarajia wa umemba katika kategoria za maneno. Makala yanabainisha kwamba kategoria ya vimahali hutegemea sifa za kisemantiki, kimofolojia na matumizi yake katika tungo. Hitimisho la makala haya ni kwamba vimahali ni maneno yenye mwingiliano wa kikategoria.
Maneno Muhimu
Vimahali, vielezi, nomino, chagizo, kiima, yambwa, kijalizo
Details

Primary Language
Kiswahili

Subjects

Journal Section
Research Article

Authors
Fabiola Hassan

Publication Date
2021-03-09

Submission Date
0000-00-00

Acceptance Date
0000-00-00

Cite

APA
Fabiola Hassan. (2021). Kategoria ya Vimahali katika Lugha ya Kiswahili. Ruaha Catholic University Journal of Education and Development, 1(1), 254-278.content_copy

Copyright © 2025 RUCU, All Rights Reserved.