RESEARCH ARTICLE
descriptionPDFMbinu na Nafasi ya Tafsiri katika Uundaji
wa Istilahi za Sayansi na Teknolojia:
Mifano Kutoka Progaram za Klinux na
Microsoft
Year 2021, Volume: 7, Issue: 2, 43-52, 2016-12-02
Hadija Jilala
Ikisiri
Makala hii inahusu tathmini ya mbinu na
nafasi ya tafsiri katika uundaji wa istilahi za
sayansi na teknolojia kwa kutumia mifano
kutoka katika programu za Klinux na
Microsoft zilizotafsiriwa kutoka Kiingereza
kwenda Kiswahili. Utafiti huu ulibaini mbinu
za tafsiri ambazo zimetumika katika uundaji
wa istilahi za sayansi na teknolojia na nafasi
ya tafsiri katika uundaji wa istilahi za sayansi
na teknolojia. Data za makala hii
zilikusanywa kwa kutumia mbinu mbili za
ukusanyaji wa data ambazo ni mbinu ya
usomaji wa machapisho na mbinu ya usaili.
Nadharia ya Ulinganifu wa aina ya matini
iliyoasisiwa na Leiss ilitumika katika
uchambuzi na uwasilishaji wa data. Makala
hii imebaini mbinu zinazotumika na nafasi
yake katika uundaji wa istilahi za sayansi na
teknolojia ambapo mbinu hizo pia hutumika
katika kupata istilahi za maneno na maana
mpya katika lugha lengwa. Makala hii
inahitimisha kuwa uundaji wa istilahi za
sayansi na teknolojia unategemea nadharia na
mbinu za tafsiri ili kupata maana na matumizi
ya istilahi za lugha chanzi katika lugha
lengwa. Hivyo, tafsiri ni daraja na nyenzo
muhimu katika uundaji wa istilahi mpya
ndani ya jamii hususan istilahi zinazotokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia.
Maneno Muhimu
Istilahi, Sayansi, Teknolojia, Klinux na Microsoft.
Details
Primary Language
Kiswahili
Journal Section
Research Article
Publication Date
2016-12-02
Submission Date
0000-00-00
Acceptance Date
0000-00-00
Cite