RESEARCH ARTICLE
descriptionPDFMatumizi ya Lugha Yanavyoibua Dhamira
katika Ushairi wa Kiswahili
Year 2022, Volume: 1, Issue: 1, 1-16, 2022-02-10
Charles Mbiu
Ikisiri
Makala hii imechunguza matumizi ya lugha
yanavyoibua dhamira katika ushairi wa Kiswahili.
Utafiti huu umefanywa kwa kurejelea diwani mbili,
yaani Wasakatonge (2003) na Chini ya Mwembe
(2017). Data za msingi za makala hii zilipatikana
maktabani kwa mbinu ya usomaji makini na
uchambuzi wa nyaraka. Matokeo ya utafiti uliozaa
makala hii yameonesha jinsi kipengele cha lugha
kinavyoibua dhamira katika diwani teule. Vipengele
vya lugha vilivyowasilishwa vilikitwa katika
mazingira, historia na utamaduni wa jamii
iliyomkuza na kumlea mwandishi. Pia, imeonesha
kuwa lugha na dhamira ni vipengele
vinavyotegemeana na kukamilishana katika kazi ya
fasihi. Makala hii inapendekeza kuwa serikali itunge
kanuni na sheria kali ili kudhibiti matumizi ya lugha
ya fasihi za kigeni zisizoendana na uhalisia wa
mazingira ya Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Maneno Muhimu
Matumizi ya Lugha, Dhamira na
Ushairi wa Kiswahili.
Details
Primary Language
Kiswahili
Journal Section
Research Article
Publication Date
2022-02-10
Submission Date
0000-00-00
Acceptance Date
0000-00-00
Cite