RESEARCH ARTICLE
descriptionPDFKufungamana kwa Vitendawili vya Wanyakyusa na Matukio
ya Kijamii
Year 2016, Volume: 2, Issue: 1, 84-95, 2016-12-02
Gerephace Mwangosi
Ikisiri
Makala haya yanahusu jinsi vitendawili vya Wanyakyusa vinavyosawiri na
kufungamana na mabadiliko yanayotokea katika muktadha halisi wa jamii
hiyo. Data ya makala haya ilikusanywa makaazini kwa mbinu ya mahojiano
na hojaji ambapo utafiti ulifanyika katika wilaya ya Rungwe. Nadharia
iliyotumika ni ile ya Uhistoria Mpya. Kanuni ya msingi katika nadharia hii
ni kuitalii fasihi, na kuikita katika muktadha wa kihistoria na kuuelewa
utamaduni na historia yake kupitia kazi za kifasihi. Historia ya jamii ni zao
la utamaduni mahususi kwa kuyachukua matukio ya kihistoria na kuyafanya
sehemu ya kazi ya fasihi (Abrams, 1999; Wamitila, 2002; Selden na
wenzake, 2005). Kwa jumla makala haya, yanalenga kuchambua vitendawili
vya Wanyakyusa vinavyofungamana na matukio ya kijamii.
Maneno Muhimu
Kufungamana kwa Vitendawili, Wanyakyusa
Details
Primary Language
Kiswahili
Journal Section
Research Article
Authors
Gerephace Mwangosi
Publication Date
2016-12-02
Submission Date
0000-00-00
Acceptance Date
0000-00-00
Cite