RESEARCH ARTICLE
descriptionPDFUchimuzi wa Fikra za Kijaala katika Ushairi wa
Kiswahili: Mifano Kutoka Tungizi za Mnyagatwa
na Diwani ya Midulu
Year 2022, Volume: 1, Issue: 1, 17-33, 2022-02-10
Hassan R. Hassan
Ikisiri
Makala hii imechunguza fikra za kijaala
zinazosawiriwa katika ushairi wa Kiswahili. Makala
imetokana na utafiti wa kimaktaba. Data
zilipatikana kwa njia ya usomaji na uchambuzi wa
matini mbalimbali na kuchambuliwa kwa kutumia
mbinu ya usimbishaji wa maudhui. Matokeo
yamewasilishwa na kujadiliwa kwa kutumia
nadharia ya Ujaala. Matokeo yanaonesha kuwa
diwani teule zilizochunguzwa zimesawiri fikra za
kijaala kupitia mianzo na miisho ya mashairi, falsafa
kuhusu uwezo wa kutunga mashairi na mielekeo ya
vipengele vya kimaudhui vinavyohusu uhai, ndoa,
uzazi, ibada na kifo. Makala hii inapendekeza
kufanyika kwa uchunguzi zaidi kuhusu uwezo na
kiasi cha tanzu nyingine za fasihi ya Kiswahili
kusawiri ujaala. Pia, uchunguzi unaweza kufanyika
ili kulinganisha uwezo na kiasi cha usawiri wa
ujaala kati ya fasihi na tawi lingine lolote la sanaa
au baina ya fasihi ya jamii ya Waswahili na ya nje
ya jamii ya Waswahili.
Maneno Muhimu
Uchimuzi, ujaala, ushairi, fikra, falsafa na itikadi.
Details
Primary Language
Kiswahili
Journal Section
Research Article
Publication Date
2022-02-10
Submission Date
0000-00-00
Acceptance Date
0000-00-00
Cite