RUAHA CATHOLIC UNIVERSITY

Ruaha Catholic University Journal of Education and Development (RUCUJED)

RESEARCH ARTICLE
descriptionPDF
Muakiso wa Uhalisi wa Kauli za Mhusika Mlevi katika Fasihi ya Kiswahili
Year 2021, Volume: 1, Issue: 1, 216-237, 2021-03-09
Lazaro Mlelwa
Ikisiri
Tamthiliya ya Kiswahili ni miongoni mwa kazi za kisanaa zenye wajibu mkubwa wa kuijenga jamii katika hali mbalimbali kupitia wahusika wake. Kwa kawaida, wahusika hudhibitiwa na kuathiriwa kwa kiasi kikubwa na muktadha wa utunzi, hasa mawazo yanayowahusu waandishi kulingana na falsafa zao, mazingira yao, utamaduni wao, hali ya maisha na harakati zilizopo katika jamii inayohusika. Makala haya yanachunguza muakiso wa uhalisi wa kauli za mhusika mlevi katika kazi za kifasihi. Zaidi pia, kuna urejeleaji watamthiliya teule za Lina Ubani (1984) na Mabepari wa Bongo (2007). Data za msingi za makala haya zimepatikana maktabani kwa kudurusu tamthiliya teule zilizobainishwa. Mapitio ya nyaraka zilizotumika kuthibitisha data za msingi pia zimepatikana kwa mbinu za usomaji wa nyaraka. Uchambuzi na mjadala wa data zilizowasilishwa umeongozwa na nadharia ya Ucheshi. Makala haya yanahitimisha kuwa mhusika mlevi ni mojawapo ya mawakala wa kazi za kifasihi kwa kuwa huyafichua na kuyaweka wazi mambo yote yanayoshindikana kusemwa na wahusika wakiwa katika ungā€˜amuzi tambuzi.
Maneno Muhimu
Muakiso, Mlevi, Mhusika, Ucheshi, Tamthiliya ya Kiswahili
Details

Primary Language
Kiswahili

Subjects

Journal Section
Research Article

Authors
Lazaro Mlelwa

Publication Date
2021-03-09

Submission Date
0000-00-00

Acceptance Date
0000-00-00

Cite

APA
Lazaro Mlelwa. (2021). Muakiso wa Uhalisi wa Kauli za Mhusika Mlevi katika Fasihi ya Kiswahili. Ruaha Catholic University Journal of Education and Development, 1(1), 216-237.content_copy

Copyright © 2025 RUCU, All Rights Reserved.