RESEARCH ARTICLE
descriptionPDFKiamu na Usomi wa Kale wa Waswahili
Year 2021, Volume: 7, Issue: 2, 20-28, 2016-12-02
Dennis Simiyu
Ikisiri
Makala hii imechunguza nafasi ya lahaja ya
Kiamu kama lugha ya usomi baina ya
Waswahili katika Pwani ya Afrika Mashariki
kabla ya kuja kwa wageni na kusanifishwa
kwa Kiswahili. Utafiti huu ni wa kimaktaba
ambapo data za msingi zimepatikana kwa
mbinu ya kimaktaba. Uchambuzi wa data
umeongozwa na nadharia ya Daiglosia.
Matokeo ya makala hii yanaonesha kuwa
lahaja ya Kiamu ndiyo ilipewa hadhi ya juu
ya kutumika kama lugha ya usomi wa
Waswahili katika jamii za Afrika Mashariki.
Pia, inahitimisha kuwa lahaja ya Kiamu ni
lahaja muhimu katika historia na maendeleo
ya jamii ya Waswahili na matumizi yake
katika nyanja za sarufi, fasihi na uandishi
zilitumiwa kuipa sifa ya kitaaluma kazi
inayohusika. Makala hii inapendekeza kuwa
Kiamu kutumika katika usomi wa kale wa
jamii ya Waswahili kabla ya usanifishaji wa
Kiswahili haina maana kwamba lahaja ya
Kiamu ilikuwa bora kuliko lahaja zingine bali
ilipewa tu hadhi ya kutumika katika shughuli
za usomi. Uchunguzi zaidi kuhusu matumizi
ya Kiamu katika visiwa vya Komoro, Unguja
na sehemu za Kongo ni muhimu.
Maneno Muhimu
Lugha ya Usomi, Kiamu, Waswahili, Lahaja na Daiglosia
Details
Primary Language
Kiswahili
Journal Section
Research Article
Publication Date
2016-12-02
Submission Date
0000-00-00
Acceptance Date
0000-00-00
Cite