RESEARCH ARTICLE
descriptionPDFUtata katika Ufasiri wa Maana za Sitiari za
Kiswahili
Year 2022, Volume: 1, Issue: 1, 77-91, 2022-02-10
Mofart Onyoni Ayiega
Ikisiri
Makala hii imechunguza utata katika ufasiri wa
maana za sitiari za Kiswahili. Data ya makala hii
ilisakurwa mtandaoni kutoka kwa tafiti za awali,
majarida na makala kwa kuongozwa na sampuli
lengwa. Data ilikusanywa kwa kutumia mbinu ya
usomaji makini. Ili kubaini utambuzi wa msikilizaji
na msomaji ujumbe, mtafiti aliwaomba
wazungumzaji 12 wa Kiswahili kufasiri maana ya
sitiari husika kwa kuongozwa na maswali ya
mahojiano huru. Nadharia ya Semantiki Tambuzi
ilitumiwa katika uchambuzi wa data ya utafiti huu.
Matokeo ya utafiti huu yalibaini kuwa utata katika
ufasiri wa maana za sitiari za Kiswahili
husababishwa na tajriba na maarifa ya mpokeaji
ujumbe, muktadha wa matumizi ya sitiari, elimu,
taswira na mazingira ya mpokeaji ujumbe. Pia,
makala hii yameeleza namna uhamishaji wa maana
hutokea katika uundaji wa maana katika sitiari
inayohusika. Uchunguzi huu ulitambua kuwa
hakuna maana mahsusi ya sitiari kwa kuwa maana
zake huwa ni dhana zilizo akilini mwa binadamu.
Makala hii inapendekeza kwamba ni vyema sitiari
kufasiriwa bila kujikita katika maana moja.
Maneno Muhimu
Sitiari, utata, semantiki, isimu
tambuzi na uhamishaji maana
Details
Primary Language
Kiswahili
Journal Section
Research Article
Authors
Mofart Onyoni Ayiega
Publication Date
2022-02-10
Submission Date
0000-00-00
Acceptance Date
0000-00-00
Cite