RESEARCH ARTICLE
descriptionPDFMapungufu ya Kiutamaduni Yanavyoathiri Ustawi wa Mwanamke katika Jamii: Mifano Kutoka Riwaya ya Sikujua
Year 2022, Volume: 1, Issue: 1, 115-300, 2022-02-10
Ndimyake Mwakanjuki
Ikisiri
Makala hii imechunguza mapungufu ya
kiutamaduni yanavyoathiri ustawi wa mwanamke
katika jamii kwa kurejelea riwaya ya Sikujua. Data
za msingi zilipatikana katika riwaya ya Sikujua kwa
mbinu ya usomaji makini. Mbinu ya uteuzi lengwa
ilitumika kupata riwaya teule. Data za upili kwa ajili
ya kufafanua na kuthibitisha data za msingi
zilipatikana kwa mbinu ya usomaji wa nyaraka
mbalimbali. Makala yamebainisha kuwa utamaduni
ni asasi mojawapo ya iliyosheheni taarifa na sheria
zilizoeleza uhusiano usio sawa baina ya mwanamke
na mwanamke katika jamii. Mwanamke amekuwa
mhanga wa kasoro zinazoendelea kumdhalilisha na
kumdunisha mwanamke. Makala haya
yanapendekeza kuwa jamii haina budi kubadilika
kwa kuacha utamaduni unaomdhulumu mwanamke.
Serikali na taasisi zisizo za kiserikali zinapaswa
kuendelea kukemea kisheria hali yoyote inayonuia
kumdhalilisha mwanamke kwa kurejelea misingi ya
mila na desturi zilizopo katika jamii.
Maneno Muhimu
Mapungufu, Utamaduni,
Mwanamke, Riwaya na Ufeministi
Details
Primary Language
Kiswahili
Journal Section
Research Article
Authors
Ndimyake Mwakanjuki
Publication Date
2022-02-10
Submission Date
0000-00-00
Acceptance Date
0000-00-00
Cite