RESEARCH ARTICLE
descriptionPDFNyimbo za Asili Zinavyoimarisha Mafunzo ya
Jadi nchini Tanzania
Year 2022, Volume: 1, Issue: 1, 34-53, 2022-02-10
Deus Gracewell Seif
Ikisiri
Makala hii imechunguza dhamira za nyimbo za
Wakaguru katika kujenga na kuimarisha mafunzo ya
jadi nchini Tanzania. Data za msingi za makala hii
zilikusanywa uwandani kwa kutumia mbinu za
mahojiano na usaili. Utafiti ulifanyika uwandani
katika mkoa wa Morogoro, wilaya ya Gairo. Utafiti
uliozaa makala hii umebaini kuwa dhamira za
nyimbo za Wakaguru hutumiwa kama ghala
maalumu lililosheheni taarifa na maarifa yaliyopo
katika jamii. Nyimbo hizo zinasaidia kuifunza jamii
masuala ya utamaduni, siasa na uchumi wa jamii
hiyo kutoka kizazi kimoja hadi kizazi kingine.
Misingi ya mila, desturi, falsafa, historia na
maendeleo yao yanarejelewa katika vipengele vingi
vya maisha yao ya jadi. Pia, hutumika kama kiungo
thabiti cha kiasili kinachojenga mfumo wa kuifunza,
kuiimarisha na kuiweka jamii pamoja katika misingi
ya utamaduni na falsafa nzima ya maisha tangu kale
mpaka sasa. Makala hii inapendekeza kuwa
ufundishwaji wa fasihi za jadi utolewe na taasisi
husika na zifanyiwe tarijama kwa ajili ya vizazi
vilivyopo na vijavyo. Pia, serikali itunge kanuni kali
za kudhibiti matumizi ya fasihi za kigeni
zisizoendana na uhalisi wa mazingira ya kiasili,
zikiwemo kanda za picha za utupu.
Maneno Muhimu
Nyimbo za kiasili, nyimbo za
Wakaguru na mafunzo ya Jadi.
Details
Primary Language
Kiswahili
Journal Section
Research Article
Authors
Deus Gracewell Seif
Publication Date
2022-02-10
Submission Date
0000-00-00
Acceptance Date
0000-00-00
Cite