RESEARCH ARTICLE
descriptionPDFNafasi ya Ontolojia ya Kiafrika katika
Jamii ya Wanyakyusa Nchini Tanzania
Year 2021, Volume: 7, Issue: 2, 62-73, 2016-12-02
Gerephace Mwangosi
Ikisiri
Makala hii imechunguza nafasi ya ontolojia ya
Kiafrika kwa kurejelea jamii ya Wanyakyusa
nchini Tanzania. Data za msingi zilipatikana
kwa mbinu ya mahojiano na usaili katika
wilaya ya Rungwe na halmashauri ya
Busokelo. Nadharia ya Usosholojia ilitumika
katika uchambuzi na mjadala wa data
zilizowasilishwa. Matokeo ya makala hii
yanaonesha umuhimu wa ontolojia ya
Kiafrika katika kuijenga na kuiendeleza
misingi imara ya kimaadili, kifalsafa na
kiutamaduni ili kuyakabili maisha na
mazingira yao. Pia, inatazamwa kama
maktaba mahsusi ya ufafanuzi na urejelezi wa
masuala ya kiasili na kiutamaduni
yanayotumika kama kiungo thabiti cha kiasili
kinachojenga mfumo wa kuifunza, kuimarisha
na kuiweka jamii pamoja katika misingi imara
ya kimaisha na kimazingira. Makala hii
inahitimisha kuwa falsafa ya Kiafrika
imejikita katika masuala ya kiontolojia ya kila
jamii kwa kuchunguza hali, kanuni za uhalisi,
chimbuko, kanuni na hatima ya kuwapo kwa
watu, vitu au maumbile.
Maneno Muhimu
Ontologia ya Kiafrika, Wanyakyusa, Utamaduni na Falsafa ya
Kiafrika.
Details
Primary Language
Kiswahili
Journal Section
Research Article
Authors
Gerephace Mwangosi
Publication Date
2016-12-02
Submission Date
0000-00-00
Acceptance Date
0000-00-00
Cite