RESEARCH ARTICLE
descriptionPDFMatumizi ya Tanakali Sauti katika Nyimbo/Misemo/Masimulizi ya Matambiko ya Jamii ya
Wabena Nchini Tanzania
Year 2024, Volume: 9, Issue: 1, 77-89, 2024-02-02
Leopard Jacob Mwalongo
Ikisiri
Makala hii inahusu uchunguzi wa matumizi ya tanakali sauti kwenye matambiko ya jamii ya
Wabena mkoani Njombe nchini Tanzania. Data za msingi zilizotumika katika makala hii
zilipatikana kwa mbinu ya mahojiano na usaili katika wilaya ya Njombe Mjini na Njombe
Vijijini, mkoani Njombe. Kijiji cha Luponde na Lusitu (Kata ya Luponde) Ihalula na Lugenge
(Kata ya Utalingoro) ndivyo vilivyolengwa katika wilaya ya Njombe Vijijinii. Kwa upande wa
Njombe Mjini, vijiji vilivyolengwa ni Mjimwema na Joshoni (Kata ya Mjimwema) Idundilanga
na Ramadhani (Kata ya Njombe mjini.). Uchambuzi wa data uliongozwa na nadharia ya
Uhalisiajabu. Makala hii imebaini kuwa matambiko ya jamii ya Wabena yamesheheni matumizi
ya tanakali sauti ambazo zinatumika kwa malengo mbalimbali yakiwemo yanayohusu kuweka
msisitizo na kusawiri uhalisi wa jambo fulani katika jamii ya Wabena. Pia, yamebaini kwamba
matambiko yana namna tofauti tofauti za matumizi ya vipengele vya lugha lengo maalumu kwa
kurejelea muktadha mahususi wa tambiko teule. Makala hii inapendekeza utafiti zaidi juu ya
matumizi ya lugha katika matambiko mbalimbali ndani na hata nje ya nchi.
Maneno Muhimu
Matambiko, Jamii ya Wabena, Tanakali Sauti na Nadharia ya Uhalisiajabu
Details
Primary Language
Kiswahili
Journal Section
Research Article
Authors
Leopard Jacob Mwalongo
Publication Date
2024-02-02
Submission Date
0000-00-00
Acceptance Date
0000-00-00
Cite