RESEARCH ARTICLE
descriptionPDFAkisiko la Hali na Mtazamo Hasi wa Maendeleo ya Mwanamke katika Jamii:
Mifano Kutoka katika Riwaya ya Wasifu wa Siti Binti Saad
Year 2023, Volume: 8, Issue: 2, 60-70, 2023-02-02
Hadija Rashid Utukulu
Ikisiri
Makala haya yamechunguza hali na mtazamo hasi wa maendeleo ya mwanamke katika jamii
kwa kurejelea riwaya ya Kiswahili.Data za msingi zimepatikana katika riwaya ya Wasifu wa Siti
Binti Saad kwa mbinu ya usomaji makini. Mapitio ya nyaraka zilizotumika kufafanua data za
msingi zilipatikana kwa mbinu za kieletroniki na kimaktaba.Uchambuzi na mjadala wa data
zilizowasilishwa uliongozwa na nadharia ya Ufeministi.Makala haya yanaelezea namna
mwanamke anavyoakisiwa katika shughuli mbalimbali za kijamii kupitia utanzu wariwaya ya
Kiswahili. Aidha, inadokeza hali halisi ya maisha na matokeo ya harakati za mwanamke pamoja
na namna jamii inavyomtazama katika maisha yake ya kila siku. Makala haya yanalenga
kuchochea mwamko thabiti wa fikira zake ili kunyanyua na kutetea nafasi, hadhi na thamani ya
kiutu anayostahiki katika ngazi na asasi mbalimbali za kijamii. Makala hii inahitimisha kuwa
mwanamke hapaswi kutazamwa katika hali ya kupuuzwa na kukandamizwa badala ya
kumtazama kama mhimili thabiti katika mifumo ya malezi, uzalishaji mali na uchumi katika
ngazi zote za jamii na taifa.
Maneno Muhimu
Hali, Hadhi, Mtazamo Hasi, Mwanamke na Fasihi ya Kiswahili
Details
Primary Language
Kiswahili
Journal Section
Research Article
Authors
Hadija Rashid Utukulu
Publication Date
2023-02-02
Submission Date
0000-00-00
Acceptance Date
0000-00-00
Cite