RUAHA CATHOLIC UNIVERSITY

Ruaha Catholic University Journal of Education and Development (RUCUJED)

RESEARCH ARTICLE
descriptionPDF
Matumizi ya Lugha Hasi Yanavyoathiri Malezi ya Watoto, Ujifunzaji na Mustakabali wa Maisha Yao
Year 2024, Volume: 3, Issue: 2, 59-76, 2024-12-02
Rose Sekile, Sebastian Nyerere Mbwillow
Ikisiri
Makala haya yanahusu matumizi ya lugha katika malezi yanavyoathiri ujifunzaji na mustakabali wa maisha yao. Kimsingi, makala yanalenga kujadili matumizi ya lugha hasi katika malezi na tendo zima la ujifunzaji. Aidha, makala yanalenga kuielekeza jamii jinsi lugha ilivyo na mchango mkubwa wa kuweza kujenga utu na kumuandaa mtu bora, au mbaya, kuzindua fikra za wanajamii ili wawe na mtazamo chanya kuhusu matumizi lugha wakati wa kulea watoto. Data zilizofanikisha makala haya zilitokana na utafiti wa uwandani kwa kiasi kikubwa na kimaktaba kwa kiasi kidogo. Data za msingi zilipatikana katika jamii. Data hizi zilipatikana kwa wazazi, walimu na wanafunzi walioko shule za msingi, sekondari, na vyuo. Mbinu ya usomaji makini na upembuzi yakinifu zilitumika kupata data za msingi. Nadharia iliyoongoza uchanganuzi wa data ni Nadharia ya Ethnografia ya Mawasiliano ya Dell Hymes (1974). Makala haya yanaonesha kuwa lugha hasi zimekuwa zikizungumzwa katika miktadha mbalimbali kama nyumbani, kwenye elimu, na katika jamii. Fauka ya hayo, matumizi ya lugha hasi katika miktadha tajwa huacha athari hasi kwa watoto hasa kisaikolojia. Makala haya yanahitimisha kwa kuitaka jamii iwe na uelewa mpana kuhusu matumizi ya lugha wakati wa malezi, kwa sababu lugha inayotumika inaweza kuwaathiri watoto. Watoto ni sehemu kubwa ya jamii, na ndiyo tegemeo la uendelevu wa taifa lolote, hivyo hatuna budi kuwalea vizuri na kuwaendeleza ili waweze kutimiza ndoto zao.
Maneno Muhimu
Lugha, Malezi, Ujifunzaji, Mustakabali
Details

Primary Language
Kiswahili

Subjects

Journal Section
Research Article

Authors
Rose Sekile, Sebastian Nyerere Mbwillow

Publication Date
2024-12-02

Submission Date
0000-00-00

Acceptance Date
0000-00-00

DOI:

Cite

APA
Rose Sekile, Sebastian Nyerere Mbwillow . (2024). Matumizi ya Lugha Hasi Yanavyoathiri Malezi ya Watoto, Ujifunzaji na Mustakabali wa Maisha Yao. Ruaha Catholic University Journal of Education and Development, 3(2), 59-76.content_copy

Copyright © 2026 RUCU, All Rights Reserved.