RESEARCH ARTICLE
descriptionPDFUtelezi wa Uainishaji wa baadhi ya Maneno ya
Kiswahili: Kigezo cha Kimofosintaksia
Year 2022, Volume: 1, Issue: 1, 92-104, 2022-02-10
Elishafati J. Ndumiwe
Ikisiri
Makala hii imechunguza utelezi wa uainishaji wa
baadhi ya maneno ya Kiswahili kwa kurejelea
kigezo cha kimofosintaksia. Data za msingi za
makala hii zimekusanywa kwa kutumia mbinu ya
upitiaji nyaraka. Nyaraka zilizochunguzwa ni Kivuli
Kinaishi na magazeti ya Ijumaa na Mwananchi.
Mbinu ya uteuzi lengwa ilitumika kupata tamthiliya
na magazeti yaliyolengwa. Katika uchanganuzi wa
data tumetumia msingi wa taarifa za kileksika na za
kiuamilifu pamoja na msingi wa muundo wa
vishiriki vya kitenzi wa nadharia ya Sarufi Leksia
Amilifu. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa
baadhi ya maneno yanabadilika kutoka aina moja
kwenda nyingine. Kwa mfano, vivumishi, vielezi
vya wakati na vya mahali vinaweza kuwa nomino.
Kiwakilishi kinaweza kuwa kibainishi na kitenzijina kinaweza kuwa kitenzi au nomino. Pia,
kihusishi kinaweza kuwa kiunganishi. Makala hii
inapendekeza kuwa, kigezo cha kimofosintaksia
kinaweza kuwa suluhisho la uainishaji wa aina za
maneno katika Kiswahili kuliko vigezo vya
kimofolojia na kisemantiki.
Maneno Muhimu
Uainishaji wa maneno,
kimofosintaksia, sarufi leksia amilifu, utelezi na mwarobaini
Details
Primary Language
Kiswahili
Journal Section
Research Article
Authors
Elishafati J. Ndumiwe
Publication Date
2022-02-10
Submission Date
0000-00-00
Acceptance Date
0000-00-00
Cite