RESEARCH ARTICLE
descriptionPDFUfutuhi kama Mbinu ya Kuwasilisha Dhamira
za Kisiasa katika Katuni za Mtandaoni za
Masoud Kipanya
Year 2022, Volume: 1, Issue: 1, 54-65, 2022-02-10
Majuto Kapaya Manyuka
Ikisiri
Makala hii inashughulikia ufutuhi katika katuni za
kisiasa za Masoud Kipanya. Kilichochunguzwa
hapa ni mbinu za ufutuhi katika katuni za kisiasa na
namna zinavyowasilisha mawazo ya kisiasa katika
jamii ya Tanzania. Data za msingi zilikusanywa
maktabani kwa mbinu ya uchanganuzi matini wa
katuni zilizochapishwa katika akaunti ya Masoud
Kipanya katika mtandao wa kijamii wa Instagram.
Data za upili kwa ajili ya ufafanuzi wa data za
msingi zilipatikana kwa mbinu ya usomaji wa
nyaraka. Nadharia ya Semiotiki imetumika ili
kufasili ishara za katuni na mawazo ya kisiasa
yanayowasilishwa na mbinu za ufutuhi. Makala hii
imebainisha kuwa katuni za kisiasa za Kipanya
hutumia mbinu za ufutuhi katika kujadili na
kuwasilisha mawazo mbalimbali ya kisiasa. Mbinu
za ufutuhi ni muhimu katika kuwasilisha ujumbe
uliokusudiwa. Makala hii inapendekeza kufanyika
kwa tafiti zaidi kuhusu ufutuhi katika tanzu
mbalimbali za fasihi.
Maneno Muhimu
Ufutuhi, mbinu za ufutuhi,
katuni, katuni za kisiasa na mtandaoni
Details
Primary Language
Kiswahili
Journal Section
Research Article
Authors
Majuto Kapaya Manyuka
Publication Date
2022-02-10
Submission Date
0000-00-00
Acceptance Date
0000-00-00
Cite