RESEARCH ARTICLE
descriptionPDFUtandawazi wa Kiswahili: Kuimarika na
Kulegalega kama Lugha Rasmi ya Afrika
Year 2022, Volume: 1, Issue: 1, 105-114, 2022-02-10
Mohamed Omary Maguo
Ikisiri
Makala hii imechunguza utandawazi wa Kiswahili,
kuimarika na kulegalega kwake kama lugha rasmi
ya Afrika. Data za msingi katika makala hii
zilipatikana maktabani kwa kudurusu nyaraka
zinazohusiana na mada teule. Data za upili
zilizotumika kuthibitisha data za msingi zilipatikana
maktabani kwa mbinu ya usomaji makini. Matokeo
ya utafiti uliozaa makala hii yameonesha historia,
maendeleo na kuimarika kwa utandawazi wa
Kiswahili Barani Afrika. Pia, imeonesha sababu za
kihistoria, kisera na kisaikolojia zinazosababisha
kulegalega kwa Kiswahili kama lugha rasmi ya
Afrika. Baadhi ya mataifa yanadai kuwa lugha za
kikoloni ni vigezo muhimu vya kupima hadhi ya
taifa kiuchumi, kisayansi na kiteknolojia. Muelekeo
huu unaangukia katika kuzienzi lugha za Kikoloni
na unaambatana na jitihada za kupuuza lugha za
asili za Kiafrika kwa kuziona katika uchanga
usioweza kumudu mahitaji ya utandawazi. Makala
hii inapendekeza kuwa ni wakati muafaka kwa
mataifa ya Afrika kuunda sera ya lugha
itakayohusisha mataifa yote na itakayotekeleza kwa
vitendo. Kwa kufanya hivyo, lugha ya Kiswahili
itakuwa alama ya Uafrika na lugha rasmi ya Afrika.
Maneno Muhimu
Utandawazi, Kiswahili, lugha
rasmi, kuimarika na kulegalega
Details
Primary Language
Kiswahili
Journal Section
Research Article
Authors
Mohamed Omary Maguo
Publication Date
2022-02-10
Submission Date
0000-00-00
Acceptance Date
0000-00-00
Cite