• PRO
  • 19 Feb 2026
  • RUCU-IRINGA

MAISHA NI MAJITOLEO

unapotafakari maana halisi ya kujitoa na kulitumikia kusudi la Mungu na jamii hapa duniani, maisha ya Hayati Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo yanakuwa darasa tosha kwetu sote.

Kuanzia Kijiji cha Mwazye mkoani Rukwa mpaka kufikia kuwa kiongozi wa juu wa Kanisa Katoliki, utume wake ulikuwa ni mfano hai wa sadaka na utumishi usiochoka:

Kujiendeleza kwa ajili ya Utume: Alijitoa kusoma hadi kupata Shahada ya Uzamivu huko Roma (1976) ili kulitumikia Kanisa kwa weledi na kina.

Utiifu na Utayari: Tangu alipopewa daraja la Upadri (1971), alikubali kwa unyenyekevu kutumwa kuhudumu popote—kuanzia Nachingwea, Tunduru-Masasi, hadi kubeba jukumu zito la Askofu Mkuu wa Dar es Salaam na baadaye Kardinali (1998).

Kutumika bila kujibakiza: Alitoa nguvu, hekima, na maisha yake yote kuliongoza kundi la Mungu hadi alipostaafu rasmi mwaka 2019.

Kifo chake leo Februari 19, 2026, kinahitimisha safari yake ya kimwili, lakini urithi wa majitoleo yake utaishi ndani ya Kanisa na mioyo ya Watanzania milele. Ndiyo maana andiko hili linatukumbusha faraja kuu: "Maana nimesadiki ya kuwa wala mauti wala uzima haviwezi kututenga na pendo la Mungu — Warumi 8:38-39"

Tunapomkumbuka na kumuombea kiongozi huyu, tujiulize: Je, wewe unaweka majitoleo gani katika nafasi na wito uliopewa leo? Pumzika kwa Amani, Mwadhama.


Source: RUCU

Advertisement