CYBER CHAMPIONSHIP COMPETATION - RUCU YATINGA NUSU FAINALI
Zaidi ya wanafunzi 20 wa Ruaha Catholic University (RUCU) wameshiriki kikamilifu katika hatua ya Nusu Fainali ya mashindano ya TCRA Cyber Championship Competition 2025–2026, yanayoratibiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kufanyika kwa njia ya mtandao (online).
Ushiriki huu umewezeshwa na miundombinu imara, rafiki na ya kisasa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ya RUCU, ambayo imekuwa chachu na faida ya ziada katika kuwawezesha wanafunzi kushiriki bila vikwazo vya kiteknolojia, huku wakionyesha kwa vitendo maarifa ya darasani.
Mashindano haya yanahusisha vyuo vikuu mbalimbali nchini, ambapo wanafunzi watakaofuzu katika hatua hii ya nusu fainali watashiriki hatua ya fainali, wakiwakilisha taasisi zao na kuwania ubingwa wa kitaifa.
Source: TCRA