ELIMU KIDIJITALI, HITAJI SIYO CHAGUO -PROF. NOMBO
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.
Carolyne Nombo amesema mabadiliko ya kidijitali si chaguo
tena bali ni hitaji la lazima, kama inavyoainishwa katika Dira
ya Taifa ya Maendeleo 2050 (DIRA 2050).
Prof. Nombo ameeleza hayo Januari 14, jijini Dodoma akifun-
gua Warsha ya kujenga uelewa wa pamoja juu ya Mkakati wa
Kitaifa na matumizi ya Teknolojia za Kidijitali katika Elimu na
Miongozo yake, akisisistiza kuwa Mkakati huo utaongoza ma-
geuzi ya kidijitali katika ngazi zote za elimu.
“Teknolojia peke yake haiwezi kuleta mabadiliko ya kweli
katika elimu bila walimu wenye ujuzi na utayari wa kutumia
teknolojia za kufundishia na kujifunzia. Kwa hiyo, vyuo vya
ualimu, vyuo vikuu na taasisi zote za mafunzo zinapaswa ku-
jumuisha kwa makusudi ufundishaji wa kidijitali“ amesema
Prof. Nombo.
Source: MoEST WEEKLY