• PRO
  • 28 Feb 2026
  • Tosamanga-Iringa

ELIMU NI CHANZO CHA MAISHA

Kuelekea mwisho wa muhula wa kwanza na kuanza kwa mitihani, wanafunzi wa Ruaha Catholic University (RUCU) wameendelea kuonesha kuwa elimu wanayoipata inakwenda sambamba na maadili na huduma kwa jamii.

Katika kipindi hiki muhimu cha maandalizi ya mitihani ya mwaka wa masomo 2025/2026, walitembelea Kituo cha Watoto Yatima Tosa Maganga kilichopo Iringa, na kushiriki katika matendo ya huruma, upendo na mshikamano kwa watoto wanaolelewa kituoni hapo.

Ziara hiyo imekuwa ishara kwamba maarifa ya kweli hayaishii darasani, bali huonekana kwa vitendo.

Tunawatakia wanafunzi wetu maandalizi mema na mafanikio katika mitihani yao — wakiendelea kuthibitisha kuwa:

Elimu ni Chanzo cha Maarifa, na Maarifa ni Mwanga wa Jamii.


Source: RUCU

Advertisement