TANZIA
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Katoliki Ruaha anasikitika kutangaza kifo cha Askofu Bernardin Francis Mfumbusa, aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Katoliki Ruaha.
Askofu Mfumbusa amefariki dunia leo tarehe 14 Aprili 2026, saa 11:45 alfajiri katika Hospitali ya Benjamin Mkapa.
Kwa masikitiko makubwa, Makamu Mkuu wa Chuo anatoa pole kwa Mkuu wa Chuo, Ask. Wolfgang Pisa OFM Cap, Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania, wajumbe wa Baraza,Seneti, wafanyakazi, wanafunzi , pamoja na waumini wote wa Jimbo katoliki la Kondoa.
Chuo Kikuu Katoliki Ruaha kimempoteza kiongozi muhimu aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya taasisi hii na Kanisa kwa ujumla.
Uongozi wa Chuo utaendelea kutoa taarifa zaidi kadri mipango ya mazishi na taratibu nyingine zitakavyokuwa zinapangwa.
Raha ya milele umpe ee Bwana, na mwanga wa milele umwangazie. Apumzike kwa amani. Amina.
Source: RUCU