USHINDI WA KIHISTORIA – RUCU YANG’ARA TENA!
Chuo Kikuu Katoliki Ruaha (RUCU) kimeandika historia nyingine kwa kuibuka mshindi wa jumla katika mashindano ya TACUSU yaliyofanyika Ifakara, mkoani Morogoro – safari hii katika mchezo wa Netball!
Hii si tu ushindi wa kawaida, bali ni uthibitisho wa:
Mazingira bora ya kujifunzia
Kukuza vipaji vya wanafunzi
Nidhamu, mshikamano na ubora wa hali ya juu
Wanachuo wetu wameonyesha kuwa mafanikio si darasani tu, bali pia katika vipaji na michezo! 💪🏽
Leo, timu imekabidhi rasmi kombe kwa Makamu Mkuu wa Chuo, ambaye amewapongeza kwa dhati na kuwashukuru kwa kuwakilisha chuo vyema na kuliletea heshima kubwa kupitia michezo.
Hongera kwa timu nzima ya Netball RUCU kwa kupeperusha vyema bendera ya chuo!
Hongera kwa uongozi na wadau wote wanaoendelea kuweka mazingira rafiki kwa ukuaji wa vipaji!
RUCU – Mahali sahihi pa elimu, vipaji na mafanikio!
Source: RUCU