WAKUU WA VYUO VIKUU TANZANIA WAKUTANA RUCU
WAKUU WA VYUO VIKUU TANZANIA WAKUTANA RUCU
Chuo Kikuu Katoliki Ruaha (RUCU) kimepata heshima ya kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Tanzania Association of Private Universities (TAPU), unaowakutanisha Wakuu wa Vyuo Vikuu Binafsi nchini kwa ajili ya kujadili masuala ya kimkakati yanayolenga kuimarisha ubora wa elimu ya juu, utafiti, ubunifu, utawala bora na ushirikiano katika sekta ya elimu nchini.
RUCU, ikiwa Mwenyeji na Mwenyekiti anayemaliza muda wake wa TAPU, imeongoza kikao hicho chini ya uenyekiti wa Makamu Mkuu wa Chuo, Sr. Prof. Chrispina S. Lekule, katika kutekeleza majukumu ya msingi ya TAPU ya kuimarisha ushirikiano kati ya vyuo vikuu binafsi na kujadili mwelekeo wa maendeleo ya elimu ya juu nchini.
Kikao hicho pia kilihusisha uchaguzi wa viongozi wapya wa TAPU, ambapo Makamu Mkuu wa Dar es Salaam Tumaini University (DarTU) alichaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa TAPU, huku Makamu Mkuu wa Catholic University of Health and Allied Sciences (CUHAS), akichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti.
RUCU imewapongeza viongozi wapya waliochaguliwa na inaendelea kuthibitisha dhamira yake ya kushirikiana na vyuo vyote nchini katika kukuza ubora wa elimu ya juu, utafiti na huduma kwa jamii nchini Tanzania.
Source: RUCU