• PRO
  • 27 Apr 2026
  • RUCU-IRINGA

Ziara Maalum ya Kihistoria RUCU

Chuo kilipata heshima kubwa kumpokea Mhashamu Baba Askofu Wolfgang Pisa, OFM.Cap., Mkuu wa Chuo na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, katika ziara maalum iliyolenga kuimarisha mahusiano, kutathmini maendeleo ya kitaaluma, pamoja na kushuhudia mazingira ya kujifunzia na kufundishia.

Katika ziara hiyo, Mkuu wa Chuo alipata fursa ya kutembelea miundombinu ya chuo, kukutana na uongozi pamoja na watumishi, kuzungumza na wanafunzi, na kusikiliza uzoefu wao wa kielimu. Aidha, alishuhudia juhudi mbalimbali zinazofanywa katika kukuza ubora wa elimu.


Source: RUCU

Advertisement