ZIARA YA WALEZI WA WANAFUNZI(DEANS)
Ruaha Catholic University (RUCU) imepokea kundi la Walezi wa Wanafunzi (Deans of Students) kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini waliotembelea chuo kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na kubadilishana uzoefu katika huduma zinazowahusu wanafunzi.
Katika ziara hiyo, Deans walipata fursa ya kukutana na Makamu Mkuu wa Chuo, Sr. Prof. Chrispina Lekule, ambaye aliwakaribisha na kuwapongeza kwa mchango wao muhimu katika kuhakikisha ustawi na maendeleo ya wanafunzi. Alisisitiza umuhimu wa nafasi ya walezi wa wanafunzi katika kujenga mazingira salama na bora ya kujifunzia.
Source: RUCU